Friday, March 16, 2012

UKO WAPI LYRICS By IGNNO

UKO WAPI LYRICS


intro


IGnno hapa, Matilda, ndugu uko wapi


Verse1
Nisikize kwa makini utazunguka hadi lini, kila siku na dakika wazidi  kuzama chini,tafakari  duniani hapa tuko safarini, umepotea kwa anasa  Massiah  anakusaka
Marafiki wanafiki walio kuzunguka, shida kuibuka moyoni wahuzunika,washikaji kutoweka mengi ya kutesa, mawimbi bado mengi utavuka na kufika
giza ya kufunika masela badilika,vya dunia vita kuja tena na kupita,Massiah mlangoni anabisha anakuita,ndugu badilika usije ukajutia
wosia nakupa  akilini shikilia,majaribu mengi lakini vumilia, kwake massiah uweke yako nia,usiyafuate ya kimwili uta angamia


Chorus

uko wapi massiah anakuita,
uko wapi massiah anakuitaji,
ukowapi massiah anakuita,
uko wapi ndugu uko wapi


Verse
Uko wapi ndugu massiah anakuita, nisikize ndugu,ndugu badilika
Mbona una nafsi mbili kama wakafiri, wafanya hili kesho lile mengi ya kisiri, utavuna ulicho panda neno  inasema,maovu na mauti wafahamu tena vyema
tazama wapi unako kwenda usije ukateleza,usife moyo kwa kweli  messiah  anakupenda,mwachie yote  nini  dunia asicho weza,wanafiki wakimbie wata kupoteza,
turehemu wengi wamo ndani ya majeneza,wanasikia hawaoni  heri  makengeza,Massiah Ebeneza niwewe unaweza,kanisani kaka nasema zangu sala ,
niyeye rafiki wa dhiki na faraja,nini unacho waza usije ukajikwaza,unatafuta nini usiku huu wa manane,jiulize ni wangapi wame kata kamba,
walielezwa tuka baki tukiwatazama, haijalishi ni mangapi yame kuzidia ,messiah ataibeba yenyu misalaba ,anawapenda wote wezi hata makahaba


Chorus

uko wapi massiah anakuita,
uko wapi massiah anakuitaji,
ukowapi massiah anakuita,
uko wapi ndugu uko wapi


verse3
Kilasiku messiah anabisha, ndugu itika, anakuita,ukowapi
mambo mengi ya fanyika maishani mitaani,midomoni wameweka zao imani,labda sielewi ni patiwe mkalimani anieleze haswa ni nani mpagani
masela roho yako umeitupa namna gani,mali imewapeleka kule gizani,sidhani kama wao bado wanajitambua,hasimu na mikosi walidhani wametua
wanakesha wakilia uhai wame ua,masela ninawapa ukweli siji kwa kifua,rudini kwenye zizi yote atayatatua,kivyako unawaza pia kuwazua
majonzi wanatamani iangaze jua,ni lini ulisikia vya shetani ni vya bure,mtafute mola na vyote vita kuja,hawana amani paa zina vuja


Chorus

uko wapi massiah anakuita,
uko wapi massiah anakuitaji,
ukowapi massiah anakuita,
uko wapi ndugu uko wapi